Raisi JPM afanya uteuzi mpya wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB

UTEUZI 

Tanzania Government's photo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, leo tarehe 5 Julai, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB Prof. William Lyakurwa.
Kufuatia hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act) Sura 257, Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kufuatia mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act) Sura 1, ametengua uteuzi wa Wajumbe Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB.
Aidha, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (1) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act, Sura 257) Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ameteua wajumbe wapya wa Bodi wafuatao kwa kipindi cha miaka mitatu
⦁ Brig. Gen (Rtd) Mabula Mashauri
⦁ Dkt. Razack B. Lokina
⦁ Bi. Rose Aiko
⦁ Prof. Joseph Bwechweshaija
⦁ Bw. Said Seif Mzee
⦁ Dkt. Arnold M. Kihaule
⦁ Bw. Maduka Paul Kessy
⦁ Bw. Charles Singili

Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi unaanza tarehe leo July 5 2016.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
05 Julai, 2016.

0 Comments